VIDEO
Queen wa Ngoma ya Akadumba, Asha Salum ‘Kidoa’ amewakomalia madairekta
wa filamu Bongo wanaopenda ngono kisha watoe kazi kuwa hatakubaliananao
kirahisi na kwamba kwake ni kazi tu.
Akipiga
stori mbili-tatu na kona ya Bongo Movies, Kidoa ambaye kwa sasa
ameingia katika filamu rasmi amesema kuwa, madairekta wengi Bongo
wanaendekeza sana ngono ndiyo wampe mtu nafasi katika kucheza filamu
jambo ambalo hatakubali limtokee.
“Nimekutana
na madairekta wengi wanaoendekeza ngono kwenye kazi. Sasa nimeshaingia
kwenye filamu hivyo madairekta uchwara wataisoma namba maana hapa kwangu
ni kazi tu na si vinginevyo,” alisema Kidoa.

Post a Comment