Watu wawili wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa, kati yao wanne vibaya baà da ya basi walilokuwa wakisafiria kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Morogoro, mali ya kampuni ya BM kuligonga ubavuni lori lililokuwa likija mbele yake na kuangukia kwenye bonde pembeni ya barabara na kupinduka mara nne, katika eneo la Lubungo Mikese, barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.
ITV imefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na
kushudia majeruhi wa basi hilo la kampuni ya BM wakiletwa kwa magari
binafsi na basi jingine la kampuni hiyo, wakionekana kujeruhiwa zaidi
maeneo ya kichwani, usoni na miguuni, ambapo mwandishi alilazimika
kuweka kalamu pembeni na kusaidiana na wananchi wengine kuwabeba
majeruhi na kuwaingiza kwa madaktari kupata huduma ya kwanza,huku
vitanda vya kuwabebea vikionekana kuwa vichache ikilinganishwa na wingi
wa majeruhi, ambapo baadhi ya waliohojiwa wameeleza namna ajali hiyo
ilivyotokea na kulalamikia wizi uliofanywa na waliofika eneo la tukio
baada ya ajali.
Daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Morogoro, Francis Semwene amekiti kupokea miili ya wanaume wawili na
majeruhi 36, ambapo wanne kati yao hali zao ni mbaya na wengine
italazimika kuwakata baadhi ya viungo iwapo watashindikana kushonwa.
Source: ITV

Post a Comment