BREAKING NEWS: Shehena ya bidhaa za kutoka nje ya nchi zakamatwa mkoani Tanga.


Shehena ya bidhaa mbalimbali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi ikiwemo vipuri vya magari kutoka nchi tofauti za Pakistan, India na Ubelgiji zimekamatwa katika bandari bubu ya Kigombe iliyopo wilayani Muheza wakati zikiingizwa nchini kinyume cha sheria bila kulipiwa ushuru.

ITV imeshuhudia askari wa jeshi la polisi zaidi ya 100 wakiwa wamezingira boti zilizotumika kubeba bidhaa hizo ambapo kamimu kamanda wa polisi mkoani Tanga mratibu mwandamizi wa jeshi polisi Mayala Towo amesema shehena ya mzigo huo ni pamoja na mafuta ya kupikia kutoka Ubelgiji, sukari kutoka India na vipuri kutoka nchi za Ulaya.
Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) tawi la Tanga Bwana amekiri kuwa hali ya ukwepaji wa kodi katika bandari bubu ya Kigombe ni ya kutisha kwa sababu sehemu kubwa ya bidhaa zinazouzwa katika maduka mbalimbali katika baadhi ya maduka yaliyopo katika jiji la Tanga, Muheza na Mkinga zinatoka nje ambazo inadaiwa kuwa zimeingizwa nchini kinyume cha sheria hatua ambayo imesababisha bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani kukosa soko.
Kufuatia hatua hiyo kaimu meneja wa forodha mkoa wa Tanga Bwana Jumbe Magoti amesema wazingatia sheria zilizowekwa katika zoezi la tozo za faini kisha watataifisha vyombo vilivyotumika katika usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka kisiwani Zanzibar kuingizwa bara bila kulipiwa ushuru.

0/Post a Comment/Comments

Stay Conneted

{ads}