Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Ndatulu Sangaya miaka 33 mkazi wa kijiji cha Ipembe wilayani Igunga Tabora amefariki dunia katika mahabusu ya mahakama ya mwanzo ya Mwamashere wilayani Kishapu
Shinyanga muda mfupi baada ya kupata mdhamana kwa tuhuma za kumshambulia mtu mmoja na kumdhuru mwili wake.
Akithibitisha kifo cha mtu huyo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Mika Nyange ameeleza kuwa mnamo tarehe kumi na tano mwezi
wa kwanza mwaka huu mtuhumiwa akiwa na baba yake mzazi aitwaye Sagaya
Shishi walimshambulia mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Ipembe wilayani
Igunga na hatimaye kukimbilia wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ambapo
walikamatwa na kufikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Ukenyenge na muda
mfupi baada ya kupewa dhamana hali yake ilibadilika ghafla na kufariki
dunia.
Aidha kamanda Nyange ameeleza kuwa hali ya mtuhumiwa ilipoonekana
kuwa mbaya alikimbizwa katika zahanati ya Mwamashele tarafa ya Ukenyenge
Kishapu na kupatiwa matibabu lakini afya yake ilizidi kuwa mbaya hali
iliyosababisha kifo chake na jeshi la polisi linaendelea kufanya
uchunguzi kuhusiana na kifo hicho.
source:ITV
source:ITV

Post a Comment