Mahusiano: Jifunze Mambo yanayosababisha uhusiano kuvunjika..

 




HAKUNA kitu kinachoumiza kama uhusiano uliokuwa unatarajia kuwa utadumu kama ukivunjika. Maumivu yake huongezeka mara dufu endapo Kitendo hicho kitatokea ghafla bila kutarajia na hapo ndio wakati
mwingine husikia watu wamekuwa vichaa au hata kujiua.
Pamoja na ukweli huo, tukumbuke zipo sababu kuu zinazofanya uhusiano uliokuwa na afya kuvunjika na wakati mwingine wenza hujikuta wamefikia katika hali hiyo na hivyo kuchelewa hata kujaribu kuokoa uhusiano husika.
Katika uhusiano kila mtu anataka kupendwa, kuheshimiwa, kuaminiwa, kushirikishwa lakini kubwa zaidi ni kusikilizana bila kudharauliana. Baadhi ya mambo ambayo ni sumu yanayochangia kwa kiasi kikubwa uhusiano kuvunjika ni pamoja na suala la uaminifu.
Hapa pande zote mbili yaani wanawake na wanaume, suala hili lisipochukuliwa kwa umakini katika uhusiano, ni wazi kuwa uhusiano huo uko hatarini kuvunjika. Uaminifu ni neno pana kwa maana kwamba uhusiano unaweza kuvunjika endapo mmoja wa wenza akiwa na uhusiano wa mapenzi na watu zaidi ya mmoja.
Upande mmoja ukijua ni wazi kuwa uhusiano huo hauwezi kudumu. Lakini pia katika uaminifu uhusiano huweza kulegalega au kuvunjika endapo ndani uhusiano huo kutakuwa na kufichiana siri na udanganyifu.
Endapo mmoja wa wenza hao atabaini kuwa yale maneno matamu yote aliyokuwa akiahidiwa au kuambiwa ni uongo, huweza kuvunja uhusiano. Tatizo lingine linaloweza kusababisha uhusiano kuvunjika ni udhibiti kupita kiasi katika uhusiano.
Yaani pale mwenza anapombana na kumfuatilia mwenza wake. Wapo wenza ambao hufikia hatua ya kufuatilia kila kitu kuhusu wenza wao, kuanzia kazini, marafiki zake, akaunti zake benki, ndugu zake na hata uhuru wake. Hii ni hatari kwani ki ukweli hakuna mtu asiyetaka kuwa huru na mambo yake.
Wapo wenza wanaofikia kila wanapokutana na wenza wao kukimbilia simu, kuulizia hadi ofisini ratiba nzima ya wenza wao, mshahara ukitoka wengine wanafikia hatua ya kutaka namna fedha zilivyotumika. Kwa udhibiti huu ni wazi uhusiano utaota mbawa. Sehemu ya pili itaendelea wiki ijayo….. Kwa mawasiliano wasiliana nasi kupitia.

0/Post a Comment/Comments

Stay Conneted

{ads}