Moto mkubwa uliowaka kwa masaa manne huko darajani Zanzibar umeteketeza nyumba za familia tano na kusababsiha hasara ya mamilioni ya shilingi huku wananchi wakiendelea kuitaka serikali ikiimarishe kikosi cha zimamoto Zanzibar.
Moto huo mkubwa ulionza saa moja na nusu usiku umeteketeza nyumba
karibu tano zilizozunguka katika mtaa wa Darajani na kusababisha gharika
kubwa zawakazi wa mtaa huo ambapo walilazimika kufanya kazi ya ziada
ikiwa ni pamoja na kuwatoa watu wazima walikuwa wamo ndani ya nyumba
hizo huku moto huo ukiwaka kwa kasi kubwa kutoka nyumba moja kwenda
nyengine.
Pamoja na jitihada za kikosi cha zimamoto kufika eneo hilo bado
askari hao walionekana kuzidiwa na kasi ya moto huo kutokana na ukosefu
wa vitendea kazi vya kisasa na pia kukabiliwa na ukosefu wa maji katika
magari yao na eneo hilo la Darjani, hali iliyosababisha wakazi wa eneo
hilo kutumia maji ya majumbani na yale ya njiani kupambana na moto huo.
Uliweza kuthibitiwa ilipofika saa tano na nusu huku zoezi hilo
likisimamiwa na mkuu wa kikosi hicho cha zimamoto Zanzibar ambaye
aliweza kuhangaika kutoka sehmu moja hadi nyengine kuhakikisha moto huo
unathibitiwa na kikosi chake ambapo akizungumza na ITV amesema maeneo ya
Mjimkongwe yana changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maji na
ufinyu wa bajeti.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliongea na ITV waliweza kutoa maoni
yao ambapo wakaitaka serikali iwajenge mazingira mazuri ya kikosi
hicho.
Hili ni tukio la kwanza kubwa la ajali ya moto kutokozea Zanzibar
kwa mwaka huu ingawa nila nne kutokezea eneo hilo la Darajani katika
kipindi cha miaka 2.

Post a Comment