Mwigulu Nchemba Atumbua BONGE LA JIPU Machinjioni!!..Ni Baada ya Kufanya Ziara Ya Kushtukiza Jana Usiku na Kurudi Tena Leo Asubuhi

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Lameck Nchemba, amemfukuza kazi mkuu wa mnada wa mifugo wa Pugu, na watumishi walioshiriki kuiba ushuru wa serikali, alipoenda machinjioni hapo kukagua.

Waziri Nchemba amesema alienda machinjioni hapo kutatua kero zinazowakabili wananchi na wadau wa machinjio hayo, huku akishirikisha wizara mbili ya Afya na TAMISEMI.

“Nimerejea asubuhi ya leo kwenye machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili watumiaji wa machinjio hayo, kutokana na uwepo wa ubadhilifu wa kodi ya serikali kwenye mnada wa pugu na malalamiko kadhaa yanayogusa wananchi wanaotumia machinjio haya, nimeshirikisha wizara mbili (TAMISEMI na AFYA) kutoa majawabu ya muda mfupi na ya kudumu”, alisema Waziri Nchemba

Baada ya kufika machinjioni hapo Waziri Mwigulu Nchemba alitoa maagizo kwamba Mkuu wa mnada wa machinjioni hapo watafute kazi nyingine, na kuwataka kufika ofisi ya Katibu Mkuu wa wizara.

“Nimeagiza kuwa Mkuu wa mnada wa Pugu na watumishi waliokuwa zamu tar. 24.12.2015 na tar.01.01.2016, kuanzia sasa watafute kazi nyigine, wakati huohuo wahakikishe wanafika ofisi ya Katibu mkuu wizarani kwangu mapema Jumatatu tar.04/01/2016”, alisema Waziri Nchemba.

Pamoja na hayo Waziri Nchemba amesitisha uchukuaji wa ushuru katika eneo la mnada wa Pugu, na kutaka makusanyo ya fedha zote yafanyike machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine za EFD.

“Kuanzia sasa nimesitisha uchukuaji wa ushuru eneo la mnada wa Pugu, badala yake makusanyo yote ya fedha za serikali yatafanyika machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine za elektroniki za EFD, kwa maana hiyo mnada wa Pugu utakuwa unatumika kutoa vibali tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa mifugo inayopaswa kuchinjw”, alisema Waziri Nchemba.

Pia waziri Nchemba ametaka eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa limejengwa kwa fedha za wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe kwa ajili ya wananchi kulitumia kuhifadhia nyama.

Hatua za kuboresha miundombinu ya machinjio hayo zimeelekezwa kwa Halmashauri ya Ilala zifanyiwe kazi haraka na kwa ubora, na kutakiwa kurudishwa kwa umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo, kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi shughuli zao.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo.[​IMG][​IMG]Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.

[​IMG]Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.[​IMG]Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.[​IMG]Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjio ya Vingunguti.[​IMG]Mh:Simbachawene akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.[​IMG]Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.[​IMG]Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.[​IMG]Furaha ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya kukubali hatua alizochukua.

0/Post a Comment/Comments

Stay Conneted

{ads}