Gari la Magazeti ya Mwananchi Lapata Ajali....Wawili Wafariki Dunia Papo Hapo




WATU wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria lililobeba Magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti kwenda mkoani mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Ajali hiyo imetokea leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru kugongana uso kwa uso na gari jingine, hivyo kulazimika kuingia nyuma ya lori na kupelekea kifo chao.

Kwa mujibu wa Wakala Afisa mauzo wa magazeti ya Mwananchi Mkoa wa Iringa Alex Kadea ambae alifika Eneo la tukio ameithibitisha kutokea kwa ajari hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa matukiodaima  kuwa waliofariki dunia wote wawili walikuwa ni madereva wa Gari hilo.
 

0/Post a Comment/Comments

Stay Conneted

{ads}