Mwili wa marehemu John Mohammed baada ya kutolewa kwenye shimo la choo.
Mtu mmoja mkazi wa kata ya Nyankumbu wilayani na mkoani Geita ajulikanaye kwa jina la John Mohammed (33) kabila Mhangaza (fundi seremala) amekutwa akiwa ameuawa usiku wa kuamkia leo tarehe 01/01/2016 na watu wasiojulikana na kutupwa kwenye shimo la choo cha nyumba ya wageni iitwayo MWIBARA GUEST HOUSE iliyopo mtaa wa Elimu katika kata ya Nyankumbu Wilayani Geita.
Baba mzazi wa Marehemu Mohamed Ibrahimu akiongea na Blog hii amesema kuwa"kutokana na maelezo niliyoyapata kutoka kwa mtoto wa dada yangu ambaye alikuwa amekuja huku kwa lengo la kufundishwa kazi ya Useremala na mtoto wangu(marehemu) ni kwamba jana jioni walikuwa wanakunywa uji na watu wengine katika kijiwe kimoja jirani na mazingira yake ya kazi,mtoto wangu akamwambia huyu kijana mtoto wa dada yangu kuwa tangulia nyumbani,akabaki yeye akikusanya vifaa vyake sasa amekwenda nyumbani yule kijana hakumwona tena na kwa kuwa ilikuwa ni usiku na huku ni mgeni hakuweza kurudi kumtafuta,leo asubuhi amekuja amekuta hapa wanapofanyia kazi kuna kofia yake huyu binamu yake halafu kumetapakaa damu,sasa ndio akaanza kutoa taarifa,na pia akanipiagia simu nikawa nimekuja kwa hiyo kwa kweli siwezi kusema namhisi mtu fulani maana mi mwenyewe nipo kwenye mshangao."
Naye Bwana Hassan Malima ambaye ni mwenyekiti wa mtaa wa Elimu amesema kuwa"mimi nimekuja hapa saa moja asubuhi baada ya kupigiwa simu kuwa kuna damu nyingi sana hapo katika kijiwe cha fundi seremara inawezekana kuna tukio,ndipo tukafika pale tukaiona ile kofia ya fundi,basi tukaanza kufanya utafiti kwa kuzunguka baadae mimi niko upande wa kule juu wakanipigia simu wakaniambia njoo huku inaonekana mwili umo humu kwenye shimo la choo basi ndipo nikaja tukaona mguu na ndipo nikaondoka na kwenda kuripoti polisi."
Matukio ya mauaji mkoani Geita yamekuwa yakijirudia mara kwa mara,itakumbukwa Julai 23,2015 kuna mlinzi aliuawa maeneo ya Nyarugusu na watu wasiojulikana,mei 4,2014 mlinzi wa kampuni ya K.K SECURITY aliuawa kwa kuchinjwa akiwa eneo la kazi yake,Machi 17,2015 mlinzi mwingine aliuawa na mwili wake kufichwa ndani ya jokofu la bar,Novemba 14,2015 aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita Alphonce mawazo aliuawa mjini katoro kwa kukatwa mapanga na watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa CCM,mbali na orodha hiyo pia kumekuwapo na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi(albino).
PAULBAHEBE BLOG inaliomba jeshi la polisi mkoani Geita kufuatilia kwa makini ili kuweza kung'oa mzizi wa wahalifu
Soource: Udaku Special

Post a Comment